Hamas: Chaguo la muqawama litaendelea kuwepo madamu uvamizi utaendelea
Aug 21, 2025 07:54 UTC
Mshauri wa Vyombo vya Habari wa Mkuu wa Ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) ametangaza kuwa harakati hii itakabiliana vikali na hali zote zinazowezekana, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango wa utawala haramu wa Israel wa kukalia kwa mabavu Ukanda wa Gaza.
Tahir al-Nunu, Vshauri wa Vyombo vya Habari wa Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Hamas, amesisitiza kwamba: "Chaguo la muqawama linabakia pale pale maadamu uvamizi huo utaendelea, na ingawa takwa letu kuu ni kusimamishwa vita na kumalizika uchokozi, lakini ikiwa vita vitalazimishwa juu yetu, hatutakuwa na budi ila kutetea watu na ardhi yetu."