Utumiaji mbaya wa silaha Marekani wasababisha vifo vya watu wawili
Aug 28, 2025 08:05 UTC
Shule moja katika mji wa Minneapolis, ulioko katika jimbo la Minnesota, siku ya Jumatano, ilishuhudia maafa mengine yaliyotokana na utumizi mbaya wa silaha zilizoko mikononi mwa raia.
Wakati wanafunzi walipoingia shuleni, walishuhudia vurugu na ghasia za matumizi mabaya ya silaha, jambo lililosababisha vifo na kujeruhiwa watu kadhaa.
Afisa wa Idara ya Sheria ya Marekani amesema: 'Watu wawili waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa kwa risasi katika shule ya Kikatoliki huko Minneapolis.'