Filamu ya 'animesheni' kuhusu Palestina yatikisa hisia za walimwengu + Video
Mtengenezaji filamu mmoja Muislamu raia wa Marekani ametengeneza filamu ya 'animesheni' iitwayo "Mimi ni kutoka Palestina" na kutikisa hisia za walimwengu katika kona mbalimbali za dunia.
Mtengezaji filamu huyo Muislamu raia wa Marekani anayeitwa Iman al Zawahiri ameingia kwenye ulimwengu muhimu sana wa watoto kwa kuja na filamu ya animesheni ambayo imeleta matumaini mapya kuhusu watoto wa Palestina hasa wa Ghaza.
Animesheni hiyo imejikita zaidi katika hali wanayokumbana nayo watoto wanaoishi nje ya nchi zao za asili, yaani suala la utambulisho wao na amefanikiwa kugusa vizuri hisia za walengwa kwa namna bora ya kishairi.
Katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita, fasihi la lugha ya watoto na mabarobaro kuhusu Palestina imepiga hatua nzuri na kupata mafanikio makubwa katika nchi nyingi duniani.
Muhusika mkuu wa animesheni hiyo ni msichana mdogo anayeitwa Samida ambaye akiwa shuleni anakumbwa na mgogoro wa kisaikolojia kwani mwalimu na wanafunzi wenzake wote wanajulikana wametokea katika nchi gani na katika nukta gani hasa ya dunia. Kila mwanafunzi anapotakiwa kuonesha nchi yake katika ramani anaonesha lakini msichana Samida yeye ambaye haioni nchi yake ya Palestina katika ramani ya dunia na anashindwa kuonesha nukta ilipo nchi yake.
Mtengenezaji filamu hakugusia mateso makubwa wanayoyapata wananchi wa Palestina lakini amefikisha vizuri ujumbe unaotakiwa kupitia nyota wa animesheni yake hiyo.