Kamanda Mkuu wa IRGC: Njia ya mapigano na makabiliano na Waistikbari inaendelea
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i101286-kamanda_mkuu_wa_irgc_njia_ya_mapigano_na_makabiliano_na_waistikbari_inaendelea
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: njia ya mapigano na makabiliano na waistikbari na maadui wa Uislamu na Iran inaendelea bila ya kusitishwa hata kwa lahadha ndogo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 20, 2023 08:19 UTC
  • Kamanda Mkuu wa IRGC: Njia ya mapigano na makabiliano na Waistikbari inaendelea

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema: njia ya mapigano na makabiliano na waistikbari na maadui wa Uislamu na Iran inaendelea bila ya kusitishwa hata kwa lahadha ndogo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Fars, Meja Jenerali Hossein Salami, ameyasema hayo leo katika Kongamano la Mashahidi 3400 wa Mkoa wa Ardabil, kaskazini-magharibi mwa Iran, ambapo sambamba na kuienzi kumbukumbu ya Mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, wa Kujihami Kutakatifu, Mashahidi Walinzi wa Haram na Mashahidi wengine wa mkoa huo amebainisha kuwa, maadui wawe na uhakika kwamba wapiganaji wa Uislamu watakabiliana nao vikali zaidi katika medani tofauti na kuwashinda vibaya zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma.
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Muqawama na kusimama imara vimepelekea kushindwa maadui wa Iran na Uislamu; na sasa wanakabiliwa na mporomoko mkubwa.

Meja Jenerali Salami amesema, maadui walitumia akiba, nishati na zana zao zote kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na akabainisha kuwa, wananchi wa Iran wamepata somo kutokana na matukio ya mwanzoni mwa Uislamu na Ashura ya Imam Hussein na hawataruhusu katu historia ijirudie tena.
Kamanda Mkuu wa IRGC ameongeza kuwa: wananchi wa Iran wamethibitisha kwamba hawatasita wakati wowote ule kukabiliana na maadui na kama ilivyokuwa huko nyuma watashinda kwa kufikia vilele vikubwa vya mafanikio.../