Iran yaadhimisha miaka 37 ya Mapinduzi ya Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i1015-iran_yaadhimisha_miaka_37_ya_mapinduzi_ya_kiislamu
Mamilioni ya wananchi wa Iran leo wamemiminika mabarabarani katika miji mbalimbali ukiwemo mji mkuu Tehran, kushiriki maandamano ya kuadhimisha miaka 37 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 11, 2016 04:18 UTC
  • Iran yaadhimisha miaka 37 ya Mapinduzi ya Kiislamu

Mamilioni ya wananchi wa Iran leo wamemiminika mabarabarani katika miji mbalimbali ukiwemo mji mkuu Tehran, kushiriki maandamano ya kuadhimisha miaka 37 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Hapa Tehran waandamanaji hao wamekusanyika katika Medani ya Azadi wakiwa wamebaba mabango ya yenye picha za mwasisi wa jamhuri ya Kiislamu, Ayatullah Khomeini MA na picha za mashahidi wengine waliouawa katika harakati hizo.

Hii leo Iran inaadhimisha miaka 37 ya Mapinduzi ya Kiislamu, ambapo wananchi chini ya uongozi wa Ayatullah Ruhullah Khomeini walihitimisha kipindi cha giza totoro katika historia ya Iran kwa kuung'oa madarakani utawala wa kidikteta wa Shah Pahlavi. Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu uliashiria kuporomoka utawala wa kidhalimu na wa kifalme uliotawala Iran kwa kipindi cha miaka 2500, ukipewa uungaji mkono mkubwa kutoka Marekani na nchi nyingine za Magharibi.

Viongozi mbalimbali waandamizi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, wanazuoni, makamanda wa jeshi, matabaka tofauti ya wananchi na kadhalika wanaoshiriki maandamano hayo. Zaidi ya waandishi wa habari 5,200 wa ndani na nje ya nchi wanafuatilia maandamano ya nchini Iran ya kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Habari zaidi kuhusu maandamano na maadhimisho ya leo zitakujieni katika matangazo yetu yajayo.