Sep 20, 2023 14:08 UTC
  • Persepolis yapoteza mechi yake ya kwanza Ligi ya Klabu Bingwa Asia

Mechi za raundi ya 1 ya Ligi ya Klabu Bingwa barani Asia zilifanyika jana Jumanne.

Mabingwa wa soka wa Iran, Persepolis walikuwa wenyeji wa timu yenye wachezaji wengi nyota ya al-Nasr ya Saudi Arabia wakiongozwa na nahodha wao, Cristiano Ronado, na walishindwa kutumia vyema methali ya mcheza kwao hutunza baada ya kushindwa katika mchezo huo.

Ikicheza ugenini katika Uwanja wa Azadi jijini Tehran bila ya watazamaji, timu yaAl-Nasr ilishinda mechi hiyo kwa mabao 2:0.

Watoto wa mjini, Persepolis ya Iran, ilipata pigo la mapema baada ya fowadi mzoefu, Mehdi Torabi kulazimika kutolewa nje ndani ya dakika 10 za kwanza kufuatia jeraha, na nafasi yake kuchukuliwa na Shahab Zahedi.

Mabao ya wageni yalifungwa katika kipindi cha pili na Abdulrahman Gharib na Mohammed Qasim.

Fowadi wa Ureno, Cristiano Ronaldo alitumia dakika 90 uwanjani na nafasi yake ikachukuliwa na mchezajii mwingine dakika za lala salama.

Mchezo unaofuata wa Al Nassr utawakutanisha wakiikaribisha Istiklol kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha King Saud mjini Riyadh, huku Persepolis wakitafuta kurekebisha mambo watakaposafiri hadi Doha kumenyana na Al Duhail ambao walikuwa wametoka sare ya 0-0 na Istiklol mapema Jumanne.

Tags