Oct 11, 2023 12:37 UTC
  • Kan'ani: Sauti ya Kushindwa Wazayuni imesikiwa na walimwengu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa mauaji yanayofanywa na wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya waandishi wa habari hayatazuia kufichuliwa ukubwa wa kushindwa kwa utawala huo na jinai zake na kuongeza kuwa: Msingi unaolegalega wa utawala dhalimu na bandia wa Israel unatetereka zaidi, na sauti za kufeli na kushindwa kwake kijeshi na kijasusi imefika kwenye masikio ya walimwengu.

Katika ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii wa X, Nasser Kan'ani, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameashiria mashambulizi ya yanayofanywa na ndege za kivita za utawala wa Kizayuni huko Gaza, kuzidishwa mzingiro na kukatwa maji na umeme katika eneo hilo na kusema: Hatua za utawala wa Kizayuni za kushadidisha mzingiro, kukata maji na umeme ya watu wa Gaza, mashambulizi dhidi ya makazi ya raia na taasisi za huduma za afya, na utumiaji wa mabomu ya fosforasi dhidi ya raia ni mifano ya jinai za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya watu wa eneo hilo.

Kan'ani Chafi amesisitiza kuwa, Palestina kamwe haitasalimu amri na kuongeza kuwa: Jamii ya kimataifa, Umoja wa Mataifa na mashirika ya kutetea haki za binadamu yana jukumu la kuzuia jinai na uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wake na kuwaadhibu wahalifu hao.

Hujuma za kikatili za Israel Ukanda wa Gaza

Vyombo vya habari vya Palestina mapema jana viliripoti shambulio la anga la utawala wa Kizayuni katika jengo la "Haji Tower" katika Ukanda wa Gaza, ambalo lilikuwa na ofisi za waandishi wa habari. Kulingana na vyanzo vya ndani, waandishi kadhaa wa habari waliuawa na wengine wengi kujeruhiwa katika shambulio hilo.

Tags