Maandamano ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina yafanyika Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i103434-maandamano_ya_kuwaunga_mkono_wananchi_madhulumu_wa_palestina_yafanyika_iran
Maandamano ya wananchi wa Iran ya Kiislamu ya kuwaunga mkono wananchi waliodhulumika wa Palestina yamefanya leo kote nchini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 13, 2023 08:20 UTC
  • Maandamano ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina yafanyika Iran

Maandamano ya wananchi wa Iran ya Kiislamu ya kuwaunga mkono wananchi waliodhulumika wa Palestina yamefanya leo kote nchini.

Shirika la habari la IRNA limeripoti kuwa, katika maandamano hayo na harakati ya Umma wa Kiislamu wa Iran ya kuunga mkono oparesheni ya "Kimbunga cha Al Aqsa cha Wapalestina", wake kwa waume kwa pamoja katika maeneo mbalimbali ya Iran leo wameandamana huku wakipiga nara za mauti kwa Israel na mauti kwa Marekani katika kubainisha hasira zao dhidi ya mashambulizi ya anga ya utawala haramu wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Hujuma hizo za anga za Wazayuni zimepelekea kuuliwa shahidi idadi kubwa ya Wapalestina wakazi wa eneo hilo wakiwemo watoto na wanawake.   

Maandamano ya kuiunga mkono Palestina

Wakazi wa mji mkuu Tehran katika Ijumaa ya leo iliyonyesha mvua wamemiminika katika mitaa mbalimbali ili kuonesha mshikamano na uungaji mkono wao kwa watoto na raia wa Ghaza wasio na hatia huku wakipiga nara na shaari za mauti kwa Israel. 

Watoto wengi katika makundi mbalimbali ya kutumbuiza wamekusanyika katika maeneo mbalimbali ya barabara ya Enghelab na kuimba nyimbo za hamasa za kuwatetea wananchi madhulumu wa Ukanda wa Ghaza na kuulani utawala haramu wa Kizayuni unaouwa watoto. 

Utawala wa Kizayuni umeishambulia Ghaza kufuatia oparesheni ya Jumamosi iliyopita tarehe 7 mwezi huu ya tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina (Hamas) dhidi ya utawala ghasibu wa Israel kwa jina la "Kimbunga cha Al Aqsa." Mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ghaza yangali yanaendelea. 

Sambamba na kuendelea mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu huko Ghaza; Wizara ya Afya ya Palestina katika takwimu zake za karibuni imetangaza kuwa Wapalestina 1,572 wameuliwa shahidi na wengine zaidi ya 7,262 kujeruhiwa katika mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Ghaza.