Ali Shamkhani: Ansarullah ya Yemen imeweka mashinikizo kwenye mshipa mkuu wa Wazayuni
-
Admeri Ali Shamkhani
Mshauri wa masuala ya kisiasa wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Hatua ya kijasiri ya Ansarullah ya Yemen ya kuzuia usafirishwaji wa meli hadi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) imeweka mashinikizo katika mshipa mkuu Wazayuni.
Admeri Ali Shamkhani amezugumzia ujasiri na urijali wa Ansarullah ya Yemen na kubainisha kwamba, nchi yoyote itakayojiunga na muungano wa Marekani kukabiliana na hatua hii ni mshirika wa moja kwa moja katika mauaji ya watoto yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Asubuhi ya jana, Youssef Al-Madani, kamanda wa Mkoa wa tano wa Jeshi la Yemen alitangaza kuwa kuongezeka mashambulizi yoyote yanayofanywa dhidi ya Ukanda wa Gaza kutapelekea kuzuka mivutano na hali ya wasiwasi katika Bahari Nyekundu.
Kamanda huyo ameongezea kwa kusema: Kwa msaada wa Mwenyezi Mungu, tutapambana na nchi au kikundi chochote kitakachotutenganisha na kutuweka mbali sisi na Palestina.
Jeshi la Wanamaji la Yemen hapo awali lilikuwa limeonya kwamba litaendelea na operesheni za kijeshi dhidi ya meli na maslahi ya adui Mzayuni hadi atakapokomesha hujuma zake dhidi ya Gaza na jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina.
Uamuzi wa Yemen wa kuzuia bidhaa zote kuingia Tel Aviv kupitia Bahari Nyekundu (Bahari ya Sham) na Mfereji wa Suez hauathiri tu mauaji ya kimbari yanayotekelezwa na utawala wa Kizayuni huko Gaza na pamoja na uchumi wake, bali pia unafutilia mbali taswira bandia ya kutoshindwa kijeshi Israel iliyopandikizwa katika fikra za baadhi ya Waarabu na nchi za Magharibi