Dec 19, 2023 07:48 UTC
  • Amir Abdollahian: Ushirikiano wa karibu wa Iran na Qatar ni dhihirisho la kuaminiana kati ya nchi mbili

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amsema kuwa ushirikiano wa karibu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar katika changamoto na masuala mbalimbali ya kimataifa na kikanda unaonyesha hali ya kuaminiana iliyopo kati ya nchi mbili.

Uhusiano wa Iran na Qatar umejenga juu ya msingi wa kuheshimiana na ujirani mwema; ambapo suala la ujirani mwema na dini ya pamoja ni kati ya mambo muhimu yaliyopelekea kushuhudiwa ushirikiano huu tajwa kati ya pande mbili. Iran na Qatar ni nchi mbili za Kiislamu katika eneo muhimu na nyeti la Ghuba ya Uajemi; na misimamo ya nchi hizo kuhusu masuala muhimu ya kikanda inakaribiana.  

Hossein Amirabdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ametuma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa X akiwapongeza wananchi, serikali na Muhammad bin Abdulrahman Al Thani Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar kwa kuadhimishwa Siku ya Taifa ya nchi hiyo na kuandika: Ushirikiano wa karibu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Qatar katika changamoto na masuala mbalimbali ya kimataifa na kikanda unadhihirisha hali ya kuaminiana kati ya nchi mbli na mtaji mkubwa kwa ajili ya kukuza uhusiano wa pande mbili. 

Siku ya Taifa ya Qatar 

Uhusiano kati ya Iran na Qatar ni miongoni mwa uhusiano thabiti na wa kirafiki katika eneo la Asia Magharibi, ambao umekumbwa na mivutano michache sana. 

Tags