Kiongozi Muadhamu: Uchaguzi ndio msingi wa mageuzi na suluhisho la matatizo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i106336-kiongozi_muadhamu_uchaguzi_ndio_msingi_wa_mageuzi_na_suluhisho_la_matatizo
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja uchaguzi wa Machi 1, 2024 hapa nchini, kuwa muhimu sana, wenye maamuzi, suluhisho la matatizo na wenye kuandaa uwanja wa mageuzi.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Dec 23, 2023 08:29 UTC
  • Kiongozi Muadhamu: Uchaguzi ndio msingi wa mageuzi na suluhisho la matatizo

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameutaja uchaguzi wa Machi 1, 2024 hapa nchini, kuwa muhimu sana, wenye maamuzi, suluhisho la matatizo na wenye kuandaa uwanja wa mageuzi.

Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema hayo leo katika hadhara kuubwa ya hamasa ya maelfu ya wananchi wa mikoa ya Khuzestan na Kerman ya Iran walionana naye katika Husseiniya ya Imamu Khomeini mjini Tehran.

Akibainisha umuhimu wa kanuni na mantiki ya uchaguzi katika Jamhuri ya Kiislamu amesema: Kuwa mfumo ni wa "Jamhuri" na wa "Kiislamu", mifumo yote hiyo miwili inategemea uchaguzi na kuongeza kuwa, kwa sababu hakuna njia nyingine ya kupatikana mfumo wenye ridhaa ya wananchi katika utawala wa nchi ghairi ya kufanya uchaguzi.

Kiongozi Muadhamu amebainisha kwamba, “kutokuwepo kwa uchaguzi” hhuwa sababu ya kuanzishwa udikteta au “machafuko, ukosefu wa usalama na vurugu” na akawakosoa wale wanaowakatisha tamaa watu ili washiriki katika uchaguzi kwa njia mbalimbali na akasema: Uchaguzi ndio njia pekee iliyo sahihi na ya kweli ambayo inaweza kudhamini  mamlaka ya ya kitaifa ya watu.

 

Katika sehhemu nyingine ya hotuba yake katika hadhara hiyo Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amezungumzia kadhia ya kimataifa na Kiislamu ya Gaza na kusema: Tukio hili ni la kipekee katika nyanja mbili; kwa upande si la kawaida kwa utawala wa Kizayuni, kwa sababu ukatili huu, jinai, umwagaji damu, mauaji ya watoto wachanga, uovu, ukatili, na kurusha mabomu juu ya vichwa vya wagonjwa na hospitali ni mambo ambayo hayakuwahi kushuhudiwa; na kwa upande wa wananchi wa Palestina na wanamapambano wa Kipalestina halina mithili kwa sababu subira kama hii, kusimama kidete namna hii na kumfanya adui awe mwendawazimu ni jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa.

Ayatullah Khamenei amebainisha: Ingawa maji, chakula, dawa na mafuta hayawafikii watu hawa, lakini wao wamesimama kama mlima, na kutosalimu amri kutawafanya washinde kwa sababu Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye kusubiri, kama ambavyo tayari ishara za ushindi zimeanza kuonekana.