"Mauaji ya kimbara Gaza yamefichua dhati na unafiki wa Wamagharibi"
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema mauaji ya kimbari yanayoshuhudiwa katika Ukanda wa Gaza yameweka bayana kuwa nchi za Magharibi zinatumia suala la 'haki za binadamu' kama wenzo wa kisiasa tu.
Hossein Amir-Abdollahian alisema hayo jana katika mazungumzo yake ya simu na Ziyad al-Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Jihadul Islami ya Palestina na kuongeza kuwa, matukio ya Gaza yameanika dhati ya ukatili wa Israel na uungaji mkono wa Ikulu ya Marekani ya White House kwa mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.
Abdollahian amebainisha kuwa, "Matukio ya karibuni huko Gaza ndani ya miezi sita iliyopita, yamefichua wazi kwa dunia kwa (nara ya) kutetea haki za binadamu, haki za wanawake, na haki za watoto ni mwanasesere wa kisiasa wa Magharibi."
Ameeleza bayana kuwa, ipo haja kwa taasisi husika za kimataifa kuchukua hatua haraka iwezekanayo ili kusitisha mauaji ya kimbari ya raia wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto wa Gaza na Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran ameeleza kuwa, taasisi husika za kimataifa zinapaswa kuchukua hatua kuhakikisha kuwa misaada ya kibinadamu inatumwa haraka na bila ya vizuizi kwa wakazi wote wa Ukanda wa Gaza.
Kwa upande wake, Ziyad al-Nakhalah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Jihadul Islami ya Palestina amepongeza na kusifu moyo wa nguvu, izza na kusimama kidete muqawama wa Palestina baada ya takriba miezi sita vita vya mauaji ya kimbari vya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
Kadhalika amewapongeza viongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kusimama bega kwa bega na kuiunga mkono kambi ya muqawama inayokabiliana na utawala pandikizi wa Israel.