Saudia imefeli katika njama za kuhuisha kikundi cha munafikina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i10990-saudia_imefeli_katika_njama_za_kuhuisha_kikundi_cha_munafikina
Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC, amesema vyombo vya habari vya ajinabi vikiwemo vya Saudia vimefeli katika jitihada zao za kuhuisha kundi la kigaidi la munafikina.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 10, 2016 13:52 UTC
  • Saudia imefeli katika njama za kuhuisha kikundi cha munafikina

Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran IRGC, amesema vyombo vya habari vya ajinabi vikiwemo vya Saudia vimefeli katika jitihada zao za kuhuisha kundi la kigaidi la munafikina.

Msemaji wa IRGC Brigedia Jenerali Ramezan Sharif akizungumza Jumapili hii ameashiria kushiriki utawala wa Saudia katika maonyesho ya mitaani ya Jumamosi mjini Paris kwa lengo la kuunga mkono kundi la kigaidi la munafikina (MKO) na kusema: "Hatua hii inaonyesha namna utawala wa Aal Saud unavyoshirikiana na kundi la kigaidi la munafikina katika jinai dhidi ya taifa la Iran."

Brigedia Jenerali Ramezan Sharif pia amelaani vikali matamshi ya Turki al Faisal, mkuu wa zamani wa shirika la kijasusi la Saudia katika mjumuiko wa kundi la kigaidi la munafikina. Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amebaini kuwa, leo fikra za waliowengi duniani wanafahamu kuwa, utawala wa Saudi Arabia ni muungaji mkono mkuu wa ugaidi katika eneo la Magharibi mwa Asia na maeneo mengine duniani.

Ameongeza kuwa, makundi ya kigaidi ya munafikina, ISIS, Taliban, Al Qaeda na makumi ya makundi mengine ya kigaidi duniani yanayotenda jinai dhidi ya binadamu yameibuliwa kwa himaya ya Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na tawala zinazopinga mageuzi katika eneo.

Brigedia Jenerali Sharif amesema ndoto iliyofeli ya munafikina na njama zilizosambaratika za Saudia kuhusu Iran ni ukweli usioweza kupingika. Amesema jinai za kundi la munafikina katika kuwaua shahidi raia na maafisa wa ngazi za juu takribani 17000 Wairani ni jambo ambalo halitasahaulika katika fikra za jamii ya wanadamu na kwamba daima watachukiwa na kustahiki adhabu kali.