May 01, 2024 04:07 UTC
  • Expo 2024: Mlango wa Iran kuingia masoko ya kimataifa

Maonyesho ya 6 ya Iran ya mauzo ya bidhaa nje ya nchi, yanayojulikana kama Iran Expo 2024, yalianza hapa Tehran Aprili 27 na yanamalizika leo Mei 1.

Maonyesho hayo ni fursa nzuri ya kuarifisha bidhaa na huduma za Iran katika soko la kimataifa sambamba na kutambulisha utamaduni, sanaa na uwezo wa kisayansi wa nchi.

Maonyesho ya 2024 ni jukwaa la kipekee la kutambulisha nguvu ya kiviwanda ya Iran na pia soko lisilojulikana kwa wafanyabiashara, wenye viwanda, na muhimu zaidi, maafisa wa serikali na watunga sera za kiuchumi na kisiasa wa nchi zingine.

Maonyesho hayo ya Tehran, yanayofanyika kama sehemu ya sera ya serikali ya kuongeza mauzo yasiyo ya mafuta nje ya nchi na kupanua uwekezaji na biashara, yameshirikisha wafanyabiashara zaidi ya 2,000 kutoka nchi 85 na maafisa zaidi ya 2,500 wa kisiasa na kiuchumi kutoka nchi 119 duniani.

Rais Ebrahim Raisi akihutubu katika sherehe za ufunguzi wa maonyesho ya Iran Expo 2024

Kwa mujibu wa Mehdi Zeighami, Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Biashara na Naibu Waziri wa Viwanda, Madini na Biashara, Iran ilipokea zaidi ya maombi 3,500 kutoka kwa nchi 103 za kutaka kushiriki, lakini iliweza kuchukua takriban wafanyabiashara 2,000 kutoka nchi 85.

Shirika la Maendeleo ya Biashara la Wizara ya Viwanda, Madini, na Biashara linatarajia mikataba ya biashara ya zaidi ya bilioni 4 itatiwa saini katika maonyesho hayo ikilinganishwa na dola milioni 450 mwaka jana