May 22, 2024 02:49 UTC
  • Bendera ya Umoja wa Mataifa yapepea nusu mlingoti kuwaenzi mashahidi wa ajali ya helikopta ya Iran

Umoja wa Mataifa umepeperusha bendera yake nusu mlingoti ikiwa ni ishara ya heshima kwa wahanga wa ajali ya helikopta nchini Iran iliyowahusisha Rais Ebrahim Raisi, Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amirabdollahian na maafisa wengine wakuu.

Bendera ya Umoja wa Mataifa jana ilipepea nusu mlingoni baada ya kufanyika marasimu katika makao makuu ya umoja huo mjini New York ambako Saeid Iravani Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa na Naibu wake Zahra Ershadi walihudhuria. 

Marasimu ya kuwaenzi mashahidi Rais Ebrahim Rais, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amir Abdollahian na wenzao waliokuwa nao pamoja yalifanyika jana katika makao makuu ya UN baada ya Katibu Mkuu Antonio Guterres kuwasilisha ujumbe wa rambirambi na salamu za pole kwa wananchi wa Iran na serikali kufuatia ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili iliyopita kaskazini magharibi mwa Iran na kupelekea kufa shahidi Rais Raisi na maafisa wengine wa ngazi ya juu. 

Mashahidi Ebrahim Raisi na Amir Abdollahian

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia lilisalia kimya kwa muda wa dakika moja kabla ya kuanza mkutano wake juzi Jumatatu kuwakumbuka wahanga wote wa ajali ya helikopta nchini Iran. Hilo lilifanyika kufuatia ombi lililowasilishwa na Russia, China na Algeria kwa niaba ya nchi wanachama wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Tags