Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aarifishwa rasmi Umoja wa Mataifa
(last modified Tue, 21 May 2024 12:21:28 GMT )
May 21, 2024 12:21 UTC
  • Kaimu Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aarifishwa rasmi Umoja wa Mataifa

Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa wa Mataifa katika barua rasmi kwa Umoja wa Mataifa amewaarifisha katika taasisi hiyo ya kimataifa Kaimu Rais na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kuwa viongozi wa muda katika nyadhifa hizo.

Amir Saeid Iravani Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa amemwandikia barua rasmi Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dennis Francis Mwenyekiti wa Baraza Kuu la 78 la UN na Pedro Comisario Afonso Rais wa Baraza la Usalama la Umoja huo akiwaalirifisha kwa Umoja wa Mataifa Kaimu Rais wa Iran Mohammad Mokhber  na Ali Bagheri Kani Naibu Waziri wa Mambo ya NJe wa Iran kuwa shakhsia watakaokaimu nafasi zilizoachwa wazi na Sayyid Ebrahim Raisi na Hossein Amir Abdollahian walioaga dunia siku ya Jumapili katika ajali ya helikopta. 

Kaimu Rais wa Iran, Mohammad Mokhber 

Aidha katika dikrii iliyotolewa katikka kikao cha ngazi ya juu cha serikali Ali Bagheri Kani aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Anayehusika na Masuala ya Kisiasa ameteuliwa kuwa Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran. 

Ayatullah Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu jana Jumatatu alituma salamu za rambirambi na kutoa mkono wa taazia kufuatia kufa shahidi katika ajali ya helikopta Rais Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje na maafisa wengine aliokuwa wamefuatana nao na kumuidhinisha kwa mujibu wa katiba Mohammad Mokheber Makamu wa kwanza wa Rais kuwa msimamizi wa shughuli za serikali kwa mujibu wa ibara ya 131 ya Katiba ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kumpa jukumu la kushirikiana na viongozi wenzake wa Idara ya Mahakama na Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ili Rais achaguliwe ndani ya siku zisizozidi hamsini.  

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Sayyid Ebrahim Raisi na viongozi kadhaa aliofuatana nao akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje, Hossein Amir-Abdollahian walikufa shahidi Jumapili katika ajali ya helikopta iliyotokea katika eneo la Varzghan mkoani Azerbaijan Mashariki, wakiwa katika kazi ya kuwahudumia na kuwatumikia wananchi.