May 04, 2024 03:13 UTC
  • Nasser Kan'ani
    Nasser Kan'ani

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Nasser Kan'ani amelaani hatua ya vyombo vya dola vya Marekani ya kukandamiza kwa mkono wa chuma maandamano ya wanafunzi wanaoitetea na kuiunga mkono Palestina yanayofanyika kwenye maeneo ya vyuo vikuu vya nchi hiyo.

Kan'ani ameandika kwenye mtadao wa X: "hatua ya mamlaka za Serikali ya Marekani ya kupotosha ukweli kwa kuzielezea hasira za dhati za wanafunzi na wanakademia na maandamano yao ya malalamiko kuwa ni kilelezo cha chuki dhidi ya Wayahudi ili kuhalalisha utumiaji wa mbinu za ukandamizaji na utumiaji mabavu kuzima maandamano ya amani na mikusanyiko ya wanafunzi wanaotetea na kuunga mkono Palestina, haipunguzi ubaya wa matendo mamlaka hizo."
Ukandamizaji unaofanywa na askari wa Marekani dhidi ya wanafunzi wanaounga mkono Palestina

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameendelea kueleza: "idadi kubwa ya Wayahudi wakiwemo wanafunzi wa Kiyahudi wametangaza kuchukizwa kwao na jinai za kuchukiza za utawala wa Kizayuni na uungaji mkono wa kuaibisha wa serikali ya Marekani kwa utawala huo”.

Kan'ani ameongezea kwa kusema "kizoro cha unafiki" kimeondolewa "kutoka kwenye nyuso za watetezi wa uongo wa uhuru wa kujieleza na haki za binadamu".../

Tags