Azimio la IAEA halitadhoofisha mipango ya maendeleo ya nyuklia ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i112588-azimio_la_iaea_halitadhoofisha_mipango_ya_maendeleo_ya_nyuklia_ya_iran
Wizara ya Mambo ya Nje imelaani vikali hatua ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA, ya kupitisha azimio dhidi ya Iran, na kusisitiza kwamba hatua hiyo haitaweza kudhoofisha mipango yake ya maendeleo ya nyuklia.
(last modified 2024-06-06T00:51:29+00:00 )
Jun 06, 2024 00:51 UTC
  • Azimio la IAEA halitadhoofisha mipango ya maendeleo ya nyuklia ya Iran

Wizara ya Mambo ya Nje imelaani vikali hatua ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA, ya kupitisha azimio dhidi ya Iran, na kusisitiza kwamba hatua hiyo haitaweza kudhoofisha mipango yake ya maendeleo ya nyuklia.

Wizara hiyo imetoa matamshi hayo katika taarifa yake siku ya Jumatano baada ya Bodi ya Magavana ya IAEA kupitisha azimio hilo, ikiishutumu Jamhuri ya Kiislamu kwa kutoshirikiana vya kutosha  na wakala huo.

Taarifa hiyo imesema: "Kupitishwa kwa azimio hilo hakutaathiri azma ya Jamhuri ya Kiislamu ya kuendelea na matumizi yake ya amani ya nishati ya nyuklia na kutekeleza mipango yake ya maendeleo ya nyuklia kulingana na haki zinazotolewa kwa nchi chini ya makubaliano ya kimataifa."

Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetaja hatua hiyo ya IAEA kuwa "hatua ya kisiasa na isiyo na manufaa" na ni jaribio la baadhi ya nchi za Magharibi kutumia vibaya mifumo ya kimataifa kulenga nchi huru.

Kituo cha nyuklia cha Bushehr

Iran inasisitiza kuwa inaendesha moja ya mipango yenye uwazi zaidi ya nishati ya nyuklia kati ya wanachama wa IAEA.

Aidha Iran imeeleza mara kwa mara utayari wake wa kutatua hitilafu zake na IAEA katika fremu ya ushirikiano wa kiufundi.

Taarifa ya wizara hiyo pia imesema kuwa "Iran imejitolea kuendeleza ushirikiano wa kiufundi na wakala huo ndani ya mfumo wa haki na wajibu wake wa kimataifa kwa kuzingatia Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaya za Nyuklia (NPT) na Mkataba wa Usalama wa Kinyuklia.