Iran: US ni kizingiti katika kupatiwa ufumbuzi masuala ya ulimwengu
(last modified Fri, 19 Jul 2024 11:09:20 GMT )
Jul 19, 2024 11:09 UTC
  • Iran: US ni kizingiti katika kupatiwa ufumbuzi masuala ya ulimwengu

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amekosoa vikali maamuzi na hatua za mabavu na za upande mmoja zinazochukuliwa na Marekani katika masuala mbali mbali ya dunia akisisitiza kuwa, mwenendo huo unafanya hali ya mambo uliwenguni kuwa mbaya zaidi.

Ali Bagheri Kani ameeleza hayo katika kikao na waandishi wa habari mjini New York leo Ijumaa na kuongeza kuwa, imethibiti kuwa, mtazamo wa upande mmoja wa Marekani katika masuala ya kimataifa umeshindwa, na kwamba Washington si sehemu ya suluhu, bali ni kikwazo katika mkondo wa amani duniani.

Kani amekosoa hatua ya Marekani ya kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015, yanayojulikana rasmi kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA), na vile vile hatua ya Washington ya kuipelekea silaha Israe, wakati huu wa vita vya mauaji ya halaiki vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Kani ameeleza bayana kuwa, "Madai ya Wamarekani kwamba uchukuaji wa maamuzi wa upande mmoja unaweza kuleta amani, utulivu na usalama duniani, hayana msingi wowote."

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria muqawama kuwa nyenzo madhubuti katika eneo la Asia Magharibi, akisisitiza kuwa mrengo huo wa mapambano una jukumu kubwa katika kuleta utulivu wa kieneo, na kuwazuia Wazayuni kuzidisha mashambulizi na mauaji ya halaiki katika eneo.

Jinai za Israel Gaza kwa uungaji mkono wa Marekani

Huku akiishutumu Marekani kwa vita vya mauaji ya kimbari yanayoendelea kufanywa na Israel katika Ukanda wa Gaza, mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza umuhimu wa kushirikiana pande kadhaa ili kurejesha amani na utulivu duniani.

Ameeleza kuwa, takriban Wapalestina 20 wasio na ulinzi wanauawa au kujeruhiwa ndani ya kila saa moja huko Gaza, huku zaidi ya asilmia 80 ya maeneo ya makazi na miundombinu yote, ikijumuisha hospitali, misikiti, makanisa, vituo vya elimu, na maeneo ya kihistoria, ikiharibiwa.

Tags