Hafla ya kuapishwa Rais wa Iran kufanyika leo
(last modified Tue, 30 Jul 2024 07:40:42 GMT )
Jul 30, 2024 07:40 UTC
  • Hafla ya kuapishwa Rais wa Iran kufanyika leo

Hafla ya kuapishwa Rais mpya wa Iran inafanyika leo katika Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge).

Kwa mujibu wa kifungu cha 121 cha katiba ya Iran; hafla ya kula kiapo Rais mpya wa Iran itafanyika leo katika kikao cha wazi cha Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran kwa kuhudhuriwa na Mkuu wa Vyombo vya Mahakama na wajumbe wa Baraza la Walinzi wa Katiba la Jamhuri ya Kiislamu.

Rais mpya wa Iran atakula kiapo katika hafla ya leo kinachosema kuwa atatumia talanta na weledi wake wote katika kutekeleza majukumu aliyokabidhiwa; na mwishoni atasaini hati ya kiapo hicho.  

Shirika la habari la Iran Press limeripoti kuwa, kwa mujibu wa kanuni za ndani za Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge); baada ya sherehe za kuapishwa Rais mpya wa Iran katika muda usiopungua wiki mbili anapasa kuwasilisha mpango jumla kwa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ukiwa na majina ya mawaziri aliowapendekeza kwa ajili ya wizara mbalimbali ambao wana uzoefu na utaalamu katika fani husika ikiwa ni pamoja na wasifu wao, mipango yao ya kazi, rekodi zao za utendaji na sifa nyinginezo. 

Hafla ya kuapishwa Rais mpya wa Iran Masoud Pezeshkian itahudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka nje na ndani ya nchi; na ndio maana tangu siku kadhaa zilizopita viongozi na maafisa wa nchi mbalimbali duniani wamewasili Tehran kupitia uwanja wa ndege wa ndege wa Imam Khomeini (M.A) kwa kuzingatia desturi za nyakati tofauti na umuhimu wa kisheria wa hafla hiyo ambayo ni nembo ya mfumo wa demokrasia na kukabidhi madaraka ya nchi kwa njia ya amani. 

Baadhi ya wageni wakiwasili Tehran 

 

Tags