Aug 15, 2024 14:16 UTC
  • Bagheri Kani: Kunyamazia ukatili wa Wazayuni kunaipa kiburi zaidi Israel

Kaimu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran amesema kuwa, uzoefu unaonyesha kuwa, kimya dhidi ya ukatili wa kijeshi na kiusalama wa Wazayuni kunaufanya utawala huo muovu kuwa na jeuri zaidi.

Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Ali Bagheri Kani amesema hayo katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Japani Yoko Kamikawa  na kueleza kwamba, kuwalenga kiraia, ikiwa ni pamoja na kulipua na kuharibu shule, misikiti, hospitali na miundombinu na vifaa vingine vya miji ni mfano wa wazi mauaji ya kikatili ya raia katika Ukanda wa Gaza katika kipindi cha miezi 10 iliyopita na biila shaka hizo ni jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari ya Wapalestina yanayofanywa na utawala wa Kizayuni.

 

Aidha amesema, sababu kuu ya hali hii isiyovumilika ni misaada ya Marekani na baadhi ya nchi nyingine za magharibi kwa genge la wahalifu linalotawala Tel Aviv kwa upande mmoja na kimya na kutochukua hatua baadhi ya nchi nyingine za magharibi dhidi ya jinai ya wazi ya utawala huo wa kibaguzi kwa upande mwingine.

Katika mazungumzo hayo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Japan, Yoko Kamikawa, pia ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuongezeka kwa mivutano katika eneo la Asia Magharibi, na kutoa mwito wa kuchukuliiwa hatua za kutuliza hali na kupunguza kiwango cha mivutano kwa kuzingatia masilahi ya pande zote.