Marekani yakiri, Iran imetekeleza JCPOA
Jul 19, 2016 03:09 UTC
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amekiri kwamba, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hadi sasa imetekeleza vipengee vyote vya makubaliano ya nyuklia maaufu kwa kifupi JCPOA.
Samantha Power ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita tangu kuanza kutekelezwa makubaliano ya JCPOA, Tehran imetekeleza waziwazi majukumu yake yote kuhusu makubaliano hayo. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa, utekelezaji wa Iran makubaliano hayo ya nyuklia ni sababu ya maendeleo ya amani na usalama wa kimataifa. Power amesisitiza kuwa, wasimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki katika miradi ya kuzalisha nishati ya nyuklia nchini Iran wamethibitisha kwamba Tehran imeketekeleza vyema majukumu yake. Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jeffry Filtmen amesema kuwa Ban Ki-moon ameipongeza Iran kwa kutekeleza majukumu yake kuhusu makubaliano ya nyuklia kati ya Tehran na nchi za kundi la 5+1.Tags