Iran: Tuko tayari kuanzisha upya mazungumzo ya kuondoa vikwazo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i121738-iran_tuko_tayari_kuanzisha_upya_mazungumzo_ya_kuondoa_vikwazo
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kisheria, Kazem Gharibabadi amesema kuna misingi na fursa zinazofaa za kuanzisha tena mazungumzo na pande nyingine.
(last modified 2025-01-21T23:20:49+00:00 )
Jan 21, 2025 23:20 UTC
  • Iran: Tuko tayari kuanzisha upya mazungumzo ya kuondoa vikwazo

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kisheria, Kazem Gharibabadi amesema kuna misingi na fursa zinazofaa za kuanzisha tena mazungumzo na pande nyingine.

Akielezea utayarifu wa Iran kwa ajili ya kuanza tena mazungumzo ya kuondolewa vikwazo, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran alisema Tehran na pande za Ulaya zimekubaliana kuendelea na mazungumzo hayo.

Alipoulizwa kuhusu mwenendo wa mazungumzo kati ya Iran na Ulaya, Kazem Gharibabadi aliwaambia waandishi wa habari mjini Tehran jana Jumanne kuwa, "Kama hapo awali, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari kuanzisha tena mazungumzo ya kuondolewa vikwazo."

Akizungumzia tarehe ya duru mpya ya mazungumzo, mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iran alisema, “Tumekubali kuendelea na mazungumzo. Tutaainisha tarehe yake kupitia mashauriano tutakayofanya.”

Gharibabadi katika Mkutano wa Maadhimisho ya miaka 75 tangu Kupitishwa kwa Mikataba ya Geneva, Tehran

Amesema Iran inaamini kuwa kuna fursa nzuri za mazungumzo na maelewano, na kuongeza kuwa, "Kila mtu anajua kwamba mpango wa nyuklia wa Iran ni wa amani na kwamba vikwazo vya upande mmoja na haramu havijafikia malengo yake."

"Njia ya busara zaidi ni kuanza mazungumzo ya kuondoa vikwazo dhidi ya Iran," amesisitiza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Masuala ya Kisheria