Miradi ya nyuklia ya Iran inaweza kuangamizwa?
Kuna swali jepesi linaloulizwa lakini muhimu; nalo ni: kwa nini mpango wa nyuklia wa Iran hauwezi kuangamizwa, tena hata kwa shambulio la kijeshi?
Viongozi wa Iran wamesikika mara kadhaa wakisema: “mpango wa nyuklia wa Iran hauangamiziki”. Kuna ukweli gani uliofichika nyuma ya kauli hii inayotolewa kwa kujiamini?
Kwanza kabisa ni kwamba, mpango na programu ya nyuklia ya Iran haiko mikononi mwa wataalamu wachache tu. Kuna maelfu ya wataalamu walioandaliwa, ambao wanafanya kazi katika sekta hiyo. Utaalamu huo wa kisayansi hauwezi kutoweka hata kwa vitisho na mauaji.
Lakini jambo la pili ni kuwa, programu ya nyuklia ya Iran imepiga hatua kufikia kiwango ambacho, haiwezekani tena kuisimamisha. Utaalamu huo, sasa hivi umegeuzwa kuwa mradi wa muundomsingi wa kitaifa; si mradi wa kupita au wa wakati fulani tu.
Nukta ya tatu ni kwamba, uwezo wa nyuklia wa Iran umefikia kiwango cha kujitosheleza kwa kila kitu cha ndani. Maana yake ni kwamba, hata kama itafungiwa njia zote, Iran haitahitaji teknolojia, wala haitakuwa na haja ya kuagizia kipuri chochote kutoka nje!
Na jambo la nne ni usalama! Kupanga njama za kujipenyeza na kufanya hujuma kwenye vituo vya nyuklia ya Iran ni kama jambo lisilowezekana. Vituo hivyo vimejengwa ndani kabisa ya milima na majabali na chini ardhi na kutawanywa kwenye kila pembe, ya eneo pana la kijiografia la Iran. Kila shambulio linaweza likapiga sehemu moja tu…lakini Iran ina makumi ya vituo....
Kkwa maelezo zaidi sikiliza makala ifuatayo: