Eslami: Iran haitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya kisiasa ya kiholela
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i127388-eslami_iran_haitasalimu_amri_mbele_ya_mashinikizo_ya_kisiasa_ya_kiholela
Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran, Mohammad Eslami amesisitiza ulazima wa kuendelea kurutubishwa Iran madini ya urani na kusema, "Watu milioni moja hutumia bidhaa zetu za dawa zenye mionzi kila mwaka.
(last modified 2025-06-09T22:47:14+00:00 )
Jun 09, 2025 22:47 UTC
  • Eslami: Iran haitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya kisiasa ya kiholela

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran, Mohammad Eslami amesisitiza ulazima wa kuendelea kurutubishwa Iran madini ya urani na kusema, "Watu milioni moja hutumia bidhaa zetu za dawa zenye mionzi kila mwaka.

Eslami amehoji kwa kusema, kwa nini tuweke afya na maisha ya watu wetu hatarini na kusalimu amri kwa mashinikizo ya kisiasa ya kiholela?"

Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Al-Arabiya, katika mkesha wa kikao cha Bodi ya Magavana wa IAEA na juhudi za Troika ya Ulaya na Marekani kupitisha azimio dhidi ya Iran kusema bayana kwamba, kila nchi ina haki, na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) una majukumu. Kwa bahati mbaya, shirika hili na taasisi nyingine za kimataifa zimepoteza uaminifu wao katika miaka ya hivi karibuni kutokana na amri na maagizo ya upande mmoja ya Marekani.

Eslami amebainisha kwamba, njia yao ya kufanya kazi imekuwa ni utekelezaji wa maagizo ya Marekani, sio sheria, kanuni na sheria za wakala huo.

Amesema kuwa hili ni tatizo linalowakabili watu wa dunia, akieleza kuwa, vigezo vya shughuli katika sekta ya nyuklia duniani kote ni sheria na kanuni zinazotumika, zinazojulikana kwa mujibu wa Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Nyuklia.

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema pia kuwa, nchi ambazo zimekuwa wanachama wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na kuridhia mkataba huu katika mabunge yao, kama vile Iran, zimejitolea na tunafanya shughuli zetu za nyuklia ndani ya mfumo huo. Eslami amesema wazi kuwa, ni jambo lisilokubalika kwa mtu yeyote kuamuru hili au lile kwa taifa kubwa la Iran.