Meja Jenerali Mousavi: Shambulio lolote tarajiwa dhidi Iran litakabiliwa kwa nguvu zaidi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i128482
Kamanda Mkuu wa Majeshi la Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi ameonya kwamba, uchokozi wowote tarajiwa wa maadui utakabiliwa na jibu baya na kali zaidi.
(last modified 2025-07-20T14:05:14+00:00 )
Jul 18, 2025 15:00 UTC
  • Meja Jenerali Mousavi: Shambulio lolote tarajiwa dhidi Iran litakabiliwa kwa nguvu zaidi

Kamanda Mkuu wa Majeshi la Iran, Meja Jenerali Abdolrahim Mousavi ameonya kwamba, uchokozi wowote tarajiwa wa maadui utakabiliwa na jibu baya na kali zaidi.

Mkuu wa Majeshi ya Iran ameyasema hayo alipotembelea Makao Makuu ya Ulinzi wa Anga ya nchi hii na kusema kuwa, "Ulinzi wa anga, katika mstari wa mbele wa kulinda anga ya nchi, umethibitisha uwezo wake wa kustahimili kiwango chochote cha tishio na utawafanya maadui wa taifa la Iran kujutia makosa yao."  

Amesisitiza kwamba, kutunguliwa kwa ndege za adui kwa wingi kunaonyesha uwezo, uimara na ushujaa wa vikosi vya ulinzi wa anga vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Meja Jenerali Mousavi ameeleza bayana kuwa, "Ulinzi wa anga, uliosimama kwenye mstari wa mbele wa ulinzi wa anga yetu, umethibitisha uwezo wake wa kustahimili viwango vyote vya vitisho na kuwafanya maadui wa taifa la Iran wajutie hesabu zao ghalati."

Mousavi ameongeza kuwa, kutunguliwa kwa idadi kubwa ya ndege za adui hakudhihirishi tu nguvu ya utendaji ya Iran bali pia azma na ujasiri wa vikosi vyake vya ulinzi wa anga.

"Idadi kubwa ya shabaha za maadui zilizopigwa chini zinaonyesha uwezo, irada, na ushujaa wa wapiganaji wetu wa ulinzi wa anga. Hii itakumbukwa katika kumbukumbu ya pamoja ya watu wa Iran," amesema Kamanda Mousavi. 

Ameongeza kuwa, "Uwezo huu, azma, Muqawama na ujasiri huu unatokana na imani isiyoyumba, fahari ya kitaifa, uongozi wa busara na usio na kifani wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, na umoja na uungaji mkono usioyumba wa watu wa Iran."

Kamanda Mkuu wa Majeshi la Iran amesisitiza kuwa, "Iwapo adui atathubutu kushambulia tena nchi yetu tunayoipenda, kwa msaada wa Mungu, atakabiliwa na mapigo makali zaidi na kushindwa zaidi ya hapo awali."