Iran ilishinda vita dhidi ya Israel na Marekani, ilimlazimisha adui akubali kushindwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i130126-iran_ilishinda_vita_dhidi_ya_israel_na_marekani_ilimlazimisha_adui_akubali_kushindwa
Kamanda mwandamizi wa kijeshi nchini Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ilishinda katika vita vya siku 12 vya kichokozi vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Israel mwezi Juni, na ilifanikiwa kumlazimisha aduia akubali kushindwa.
(last modified 2025-08-28T11:53:53+00:00 )
Aug 28, 2025 11:53 UTC
  • Iran ilishinda vita dhidi ya Israel na Marekani, ilimlazimisha adui akubali kushindwa

Kamanda mwandamizi wa kijeshi nchini Iran amesema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ilishinda katika vita vya siku 12 vya kichokozi vilivyoanzishwa na Marekani na utawala wa Israel mwezi Juni, na ilifanikiwa kumlazimisha aduia akubali kushindwa.

Mkuu wa Idara ya Utamaduni ya Majeshi ya Iran, Brigedia Jenerali Abolfazl Shekarchi, ametoa kauli hiyo katika hafla ya kuwaenzi wanahabari na wanaharakati wa vyombo vya habari Alhamisi.

Ameongeza kuwa: “Adui, huku akitumia silaha za kisasa na vita mseto kwa kiwango kamili, alijaribu kuangusha utawala wa Kiislamu ndani ya wiki moja, lakini alikosea katika makadirio yake.”
Amebainisha kuwa uimara wa taifa la Iran, uongozi wenye busara wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, na juhudi kubwa za Majeshi ya Iran ni nukta muhimu katika ushindi wa nchi dhidi ya maadui katika vita ilivyolazimishwa kupigana.
Ameongeza kuwa nchi nyingi za Magharibi ziliuunga mkono utawala wa Israel katika vita vilivyoanzishwa dhidi ya Iran, akisema hawakuwa na njia nyingine isipokuwa kupendekeza kusitishwa mapigano.
Kamanda huyo amesisitiza umuhimu wa kuzingatia vita vya kisaikolojia na vya vyombo vya habari. Amewapongeza wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini Iran na wanahabari waliowasaidia wapiganaji shujaa katika vita na hivyo kuwa na nafasi muhimu katika ushindi wa mwisho wa nchi.
Amesema wafanyakazi wa vyombo vya habari wanaweza kujenga matumaini na imani katika taifa na kuwatia hasara maadui.
Mnamo Juni 13, Israel ilianzisha shambulizi la wazi na la kichokozi dhidi ya Iran, na kuendeleza vita kwa siku 12 vilivyopelekea vifo vya watu wasiopungua 1,064 nchini Iran, wakiwemo makamanda wa kijeshi, wanasayansi wa kinyuklia na raia wa kawaida.
Marekani pia illingia katika vita kwa kulipua maeneo matatu ya nyuklia ya Iran, hatua ambayo ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.
Katika kukabiliana na uchokozi huo, Majeshi ya Iran yalishambulia maeneo muhimu ya utawala wa Israel pamoja na kambi ya kijeshi ya Marekani ya al-Udeid huko Qatar, ambayo ni kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Marekani katika Asia Magharibi.
Mnamo Juni 24, Iran, kupitia operesheni zake za kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Israel na Marekani, ilifanikiwa kuwalazimisha maadui hao kusitisha uchokozi huo wa kigaidi.