Kallas asisitiza tena kuendelezwa diplomasia ya nyuklia na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i131668-kallas_asisitiza_tena_kuendelezwa_diplomasia_ya_nyuklia_na_iran
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ambaye alielekea Kuwait kuhudhuria Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Usalama na Ushirikiano wa Kikanda kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa kutekelezwa utaratibu kwa jina la Snapback hakumaanishi kufikia kikomo diplomasia na Iran.
(last modified 2025-10-07T06:01:13+00:00 )
Oct 06, 2025 12:27 UTC
  • Kallas asisitiza tena kuendelezwa diplomasia ya nyuklia na Iran

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ambaye alielekea Kuwait kuhudhuria Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Usalama na Ushirikiano wa Kikanda kwa mara nyingine tena amesisitiza kuwa kutekelezwa utaratibu kwa jina la Snapback hakumaanishi kufikia kikomo diplomasia na Iran.

Amesema,  mazungumzo ni suluhisho pekee endelevu kwa kadhia ya nyuklia ya Iran.

Bi Kaja Kallas amesema katika tovuti rasmi ya Umoja wa Ulaya kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena wiki iliyopita liliiwekea Iran vikwazo miaka kumi baada ya kuanza kutekelezwa makubaliano ya JCPOA. 

Bila ya kuashiria masharti yasiyo ya kimantiki ya Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kwa ajili ya kuongeza muda wa utaratibu wa Snapback amedai kuwa nchi za Ulaya (E3) zilitoa fursa katika uwanja huo lakini hatua hiyo haikupelekea kuandaliwa mazingira yanayohitajika ili kurefusha muda wa azimio husika la Baraza la Usalama. 

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya aidha amesisitiza kuwa: "Hata hivyo kurejea kwa vikwazo na vizingiti vingine vya nyuklia hakupasi kuwa mwisho wa diplomasia." 

"Kwa hiyo, nitaendelea kushirikiana na pande zote husika, ikiwa ni pamoja na Iran, kwa sababu ufumbuzi wa kudumu wa kadhia ya nyuklia ya Iran unaweza kupatikana tu kupitia mazungumzo na diplomasia.

Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya amekariri madai ya kisiasa kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran inayotekelezwa kwa malengo ya amani ambapo amesema na hapa ninamnukuu: "Kwa kufanya kazi pamoja tunaweza kuhakikisha kwamba Iran inakuwa mshirika anayewajibika," mwisho wa kunukuu.