Mwakilishi wa Iran akosoa undumilakuwili wa UN
Mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran anayehusika na jamii za wachache amekosoa misimamo ya nyuso mbili na ya kindulimakuwili la Umoja wa Mataifa katika kuyaendea masuala mbalimbali duniani ambayo yanapingwa na madola ya kibeberu.
Bi Sara Fallahi aidha amekosoa undumilakuwili wa baadhi ya nchi zinazojaribu kuonesha taswira potofu kuhusu Iran na kufanya ubaguzi wa kimuundo na kimfumo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Mehr, katika siku ya kwanza ya vikao vya Bunge la 18 la Jamii za Wachache la Umoja wa Mataifa jana Alkhamisi Novemba 27, 2025, Bi Sara Fallahi alisema kuwa, akiwa mwakilishi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran analitaka bunge hilo kuona pia mafanikio ya Iran.
Ametangaza msimamo huo kwa kusoma taarifa inayotetea mafanikio ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kulinda kikamilifu haki za jamii za wachache na kukosoa misimamo ya nyuso mbili ya Umoja wa Mataifa na baadhi ya nchi zinazopotosha walimwengu na ambayo yanafanya njama za kuonesha taswira potofu kuhusu Jamhuri ya Kiislamu.
Amelalamikia pia ubaguzi wa kimuundo na kimfumo unaofanywa na madola hayo dhidi ya Iran.
Vilevile Bi Fallahi amekosoa vikali upendeleo na misimamo isiyo na msingi wa kimantiki ya baadhi ya serikali za Magharibi zinazodai kutetea haki za binadamu.
Baada ya mwakilishi wa Iran kusoma taarifa hiyo, kundi la watu mashuhuri waliokuwepo ndani ya baraza, wamemshukuru Bi Sara Fallahi na kumpokea kwa uchangamfu yeye na ujumbe ulioambatana nao. Wamepongeza misimamo imara ya Fallahi na hotuba yake iliyowagusa wengi kutokana na ukweli wake usiopingika.