Video: Duma wa Iran akiwa mawindoni
Sep 07, 2016 23:04 UTC
Miongoni mwa wanyama walio katika hatari ya kutoweka, ni duma wa Iran ambao hivi sasa wamebakia wachache sana.
Wanyama hao walikuwa wengi na wakiishi maeneo ya milimani na katika nyika. hata hivyo kwa miaka mingi sasa wako katika hatari ya kutoweka kabisa.
Uchunguzi wa hivi karibuni unaonesha kuwa, wamebakia kama duma 70 hadi 100 tu katika baadhi ya maeneo nchini Iran.
Hayo yanatokana na ushunguzi wa kijiografia uliofanywa kwa kutumia kamera zaidi ya 12,000 zenye uwezo wa kuchukua picha nyakati za usiku ambazo zilitumika kwenye maeneo tofauti ya Iran katika utafiti huo.
Tags