Boti za Kivita za Iran zazitia kiwewe meli za kivita za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i15526-boti_za_kivita_za_iran_zazitia_kiwewe_meli_za_kivita_za_marekani
Boti za kivita za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC zimezitia kiwewe na kuzidhalilisha meli za kivita za Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.
(last modified 2026-08-18T17:02:23+00:00 )
Sep 17, 2016 23:17 UTC
  • Boti za Kivita za Iran zazitia kiwewe meli za kivita za Marekani

Boti za kivita za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu IRGC zimezitia kiwewe na kuzidhalilisha meli za kivita za Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi.

Hayo yamesemwa na Meja Jenerali Mohammad Hossein Baqeri Mkuu wa Vikosi Vyote vya Ulinzi vya Iran alipokuwa akihutubia makamanda wa jeshi la SEPAH (IRGC) hapa mjini Tehran jana Jumamosi.

Ameongeza kuwa, "Vitendo vya kishujaa vya vikosi vya majini vya IRGC vimezidhalilisha meli za kivita za Marekani katika Ghuba ya Uajemi na Lango Bahari la Hormuz." Ameongeza kuwa boti za kasi za jeshi la SEPAH zimezitia kiwewe meli za kivita za Marekani.

Meja Jenerali Baqeri

Mwezi huu wa Septemba msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, Kapteni Jeff Davis alisema boti saba za kasi za wanamaji wa IRGC ziliiandama meli ya kivita ya Marekani ya USS Firebolt Septemba sita baada ya meli hiyo ya Marekani kukaribia kuingia kwenye maji ya Iran.