Salehi: Karibuni dawamiale zinazotengezwa nchini zitauzwa kwa wingi nje ya nchi
(last modified Tue, 18 Oct 2016 15:29:43 GMT )
Oct 18, 2016 15:29 UTC
  • Salehi: Karibuni dawamiale zinazotengezwa nchini zitauzwa kwa wingi nje ya nchi

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran (AEOI) amesema karibuni dawamiale (Radiopharmaceuticals) zinazotengezwa nchini zitaanza kusafirishwa na kuuzwa kwa wingi nje ya nchi.

Dakta Ali Akbar Salehi, ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo pembeni ya kongamano la taifa la "Wenye Vipawa wa Kesho" lililofanyika hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa dawamiale zinazotengezwa na wataalamu wenye vipawa wa nyuklia wa Iran zimeshafikia kiwango cha ubora wa kimataifa na kwamba hivi karibuni dawa hizo zitasambazwa kwa wingi katika masoko ya kimataifa.

Wataalamu wa Kiirani katika kiwanda cha utengezaji dawa

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki ameashiria aina 25 za dawamiale zinazozalishwa hapa nchini na kufafanua kwa kusema: "Kwa sasa dawamiale za Iran zinasafirishwa na kuuzwa katika nchi kadhaa ikiwemo Iraq, Misri na Ujerumani, lakini usafirishaji huo utaongezeka kwa kiwango cha juu baada ya kupata leseni ya ubora wa kimataifa.

Dakta Salehi ameashiria pia ujenzi wa hospitali ya kwanza ya nyuklia hapa nchini na kueleza kwamba bajeti ya fedha za kutekeleza mradi wa ujenzi huo imeshapatikana na mkataba wa ushirikiano na shirika moja la Austria juu ya suala hilo utasainiwa hivi karibuni.

Kituo cha nyuklia cha Iran

Huku akiashriia kuwa kwa sasa kuna nchi tano tu duniani zenye hospitali ya aina hiyo, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  amesema, hivi karibuni timu ya madaktari na wauguzi itapelekwa nchini Austria ili kupatiwa mafunzo yanayohitajika kabla ya kukamilika ujenzi wa hospitali hiyo.../

 

Tags