Velayati: Matamshi ya Waziri Mkuu wa Uingereza hayana athari za kivitendo
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratejia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, matamshi yaliyo dhidi ya Iran ya Waziri Mkuu wa Uingereza katika mkutano wa usalama mjini Manama nchini Bahrain hayana athari za kivitendo.
Ali Akbar Velayati amesema kuwa, matamshi ya Theresa May Waziri Mkuu wa Uingereza lengo lake ni kuipa moyo Saudi Arabia kutokana na kushindwa kwake mtawalia huko Syria na Yemen.
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratejia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, kuendelea kuiuzia silaha Saudia na makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Riyadh ni moja ya sababu za matamshi yaliyo dhidi ya Iran ya Theresa May na kubainisha kwamba, Wamagharibi ni wafanyabiashara na wanachokiangalia na maslahi yao tu.
Dakta Velayati amaeshiria hatua ya kupasishwa mpango wa kuongeza muda vikwazo dhidi ya Iran katika Kongresi ya Marekani na kusema kuwa, kuviongezea muda vikwazo hakuna tofauti na kuweka vikwazo na bila shaka hatua hiyo ya Marekani haitabakia hivi hivi bila majibu.
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratejia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran ameashiria mazungumzo yake ya leo na Ramadhan Abdallah Shallah, Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul Islami ya Palestina na kusema kuwa, pande mbili zimejadili katika mazungumzo hayo mpango wa vipengee 10 wa Jihadul Islami.
Amesema baadhi ya vipengee hivyo ni kutoutambua utawala haramu wa Israel na kubatilishwa makubaliano ya Oslo.