Dec 22, 2016 03:36 UTC
  • Marais wa Iran na Armenia wasisitiza kutekelezwa hati za makubaliano ya ushirikiano

Marais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Armenia wamesisitiza kuhusu azma ya nchi mbili ya kustawisha uhusiano wa pande mbili, wa kieneo na kimataifa.

Rais Hassan Rouhani wa Iran na mwenzake wa Armenia Serzh Sargsyan walitoa sisitizo hilo jana katika taarifa ya pamoja waliyotoa huko Yeravan, mji mkuu wa Armenia baada ya mazungumzo yao na kueleza kwamba kuna udharura wa kutekelezwa makubaliano yote yaliyofikiwa kati ya nchi mbili katika nyanja za biashara, usafirishaji, mawasiliano, viwanda na nyanja nyingine za kiuchumi.

Mapema katika mazungumzo na mwenyeji wake, Rais Rouhani alisema, kuleta amani ya kudumu na usalama katika eneo ni jambo lisiloepukika na kusisitiza kwamba ushirikiano jumuishi unahitajika ili kuweza kutatua migogoro ya eneo kwa njia ya amani na kupambana na vitendo vya ukatili na mielekeo ya kufurutu mpaka.

Rais Rouhani na mwenyeji wake Rais  Serzh Sargsyan wa Armenia

Mwishoni mwa safari ya siku moja ya Rais wa Iran nchini  Armenia, pande zmbili za Tehran na Yeravan zilitia saini hati tano za maelewano na mkataba wa ushirikiano katika nyanja za utalii, makumbusho, michezo na masuala ya mipaka.

Baada ya kumaliza safari yake ya kuitembelea Armenia Rais Rouhani jana hiyohiyo alielekea nchini Kazakhstan kuendelea na safari yake ya kuzitembelea nchi tatu za Asia ya Kati.../ 

 

 

Tags