Zarif asisitiza udharura wa kuwepo umoja na mshikamano wa Kiislamu
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i23305-zarif_asisitiza_udharura_wa_kuwepo_umoja_na_mshikamano_wa_kiislamu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kuwepo umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu
(last modified 2024-06-10T09:25:34+00:00 )
Jan 12, 2017 03:48 UTC
  • Zarif asisitiza udharura wa kuwepo umoja na mshikamano wa Kiislamu

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza udharura wa kuwepo umoja na mshikamano katika ulimwengu wa Kiislamu

Muhammad Javad Zarif ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Spika wa Bunge la Mali aliyeko safari hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, anatarajia mkutano ujao wa Jumuiya ya Mabunge ya Kiislamu utapiga hatua katika njia ya kuimarisha umoja na mshikamano wa nchi za Kiislamu kwa ajili ya kupambana na vitisho vya Umma wa Kiislamu. 

Image Caption

Kwa upande wake Spika wa Bunge la Mali, Issaka Sidibe ametoa mkono wa pole na rambirambi kutokana na kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Mfumo wa Kiislamu hapa nchini Ayatullah Hashemi Rafsanjani na kusema: Suala la kuimarisha zaidi uhusiano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lina umuhimu mkubwa kwa taifa la Mali. Spika Sidibe amesema nchi yake inalitambua taifa la Iran kuwa ni taifa ngangari na lenye azma na irada madhubuti.

Sidibe na Zarif

Katika mazungumzo hayo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Muhammad Javad Zarif na Spika wa Bunge la Mali wamejadili na kubadilishana mawazo kuhusu uhusiano wa pande mbili hasa katika upande wa masuala ya kibunge, mkutano ujao wa Umoja wa Mabunge ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) nchini Mali na umuhimu wa kushiriki Iran katika mkutano huo kama mwanzilishi wa jumuiya hiyo, suala la kupambana na kung'oa mizizi ya ugaidi na ulazima wa kuundwa kamisheni ya pamoja ya kiuchumi ya nchi hizo mbili.