Nyota wa filamu ya "Forushande" ya Iran kususia sherehe ya Oscar
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i24303-nyota_wa_filamu_ya_forushande_ya_iran_kususia_sherehe_ya_oscar
Nyota wa filamu ya Kiirani ya Forudhande ameamua kususia sherehe ya tuzo ya filamu ya Oscar huko Marekani akilalamikia hatua ya kibaguzi ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Jan 27, 2017 04:19 UTC
  • Nyota wa filamu ya

Nyota wa filamu ya Kiirani ya Forudhande ameamua kususia sherehe ya tuzo ya filamu ya Oscar huko Marekani akilalamikia hatua ya kibaguzi ya Rais wa nchi hiyo, Donald Trump.

Taraneh Alidoosti ambaye ameteuliwa kuwa mgombea wa tuzo ya filamu ya Oscar ametangza kuwa atasusia kushiriki katika sherehe ya tuzo ya Oscar kupinga na kuonesha malalamiko yake dhidi ya uamuzi wa Rais wa Donald Trump wa Marekani wa kuwazuia Waislamu kutoka baadhi ya nchi kuingia nchini humo.

Taraneh Alidoosti ameandika katika mtandao wa kijamii wa Tweeter kwamba, uamuzi wa Trump wa kuzuia visa kwa Wairani na Waislamu wa nchi nyingine kadhaa ni hatua ya kibaguzi na kwamba hatashiriki katika sherehe hiyo ili kuonesha upinzani wake dhidi ya uamuzi wa Trump.

Filamu ya The Salesman

Filamu ya Forushandeh (The Salesman) iliyotengenezwa na Asghar Farhadi imewekwa katika orodha ya filamu tano za kigeni za sherehe ya 89 za Academia ya Oscar.

Hadi sasa filamu hiyo imeshinda tuzo nyingi za kimataifa ikiwemo tuzo ya filamu bora ya Tamasha la Munich nchini Ujerumani, tuzo ya filamu bora kwa mtazamo wa wananchi ya Tamasha la Filamu la Amsterdam, Uholanzi na Tuzo ya Jumuiya ya Kitaifa ya Ukosoaji Filamu ya Marekani.