Dakta Velayati: Siasa za vitisho haziwezi kuzuia kufilisika kisiasa kwa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i24689-dakta_velayati_siasa_za_vitisho_haziwezi_kuzuia_kufilisika_kisiasa_kwa_marekani
Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratejia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, utumiaji wa siasa za vitisho unaofanywa na Marekani hauwezi kuiokoa nchi hiyo na kufilisika kisiasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2017 12:49 UTC
  • Dakta Velayati: Siasa za vitisho haziwezi kuzuia kufilisika kisiasa kwa Marekani

Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratejia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, utumiaji wa siasa za vitisho unaofanywa na Marekani hauwezi kuiokoa nchi hiyo na kufilisika kisiasa.

Ali Akbar Velayati amesema hayo leo katika mahojiano yake na Shirika la Radio na Televisheni la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambapo ameashiria vitisho vya hivi karibuni vya Marekani dhidi ya Iran na kusisitiza kwamba, hii si mara ya kwanza kwa Wamarekani kutoa vitisho vitupu na kufanya propaganda dhidi ya taifa hili.

Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratejia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, Wamarekani wanatambua vyema kwamba, Wairani hawaogopeshwi na vitisho.

Rais Donald Trump wa Marekani

Amesema, wananchi wa Iran wameonyesha kusimama kwao kidete mara chungu nzima dhidi ya vitisho na wakati mwingine katika vita kama vile vya kulazimishwa Iran vilivyoanzishwa na utawala wa dikteta Saddam Hussein, na adui hakupata faida yoyote.

Mkuu wa Kituo cha Utafiti wa Kistratejia cha Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu wa Iran amesema kuwa, kuzisaidia tawala ambazo ziko katika hali ya kusambaratika na ambazo zinaunga mkono ugaidi katika Mashariki ya Kati ikiwemo Saudi Arabia na utawala haramu wa Israel ni miongoni mwa sababu ya vitisho vya Marekani dhidi ya Iran na kuongeza kuwa, tawala hizo zimechanganyikiwa kutokana na kushindwa huko Iraq, Syria, Yemen na Lebanon.