Kamanda wa Sepah: Trump ni mwanagenzi, vitisho vya Marekani havina meno
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i24875-kamanda_wa_sepah_trump_ni_mwanagenzi_vitisho_vya_marekani_havina_meno
Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) amesema kuwa wanasiasa wa Marekani wanaelewa vyema kwamba vitisho dhidi ya Iran havina faida yoyote bali vina madhara.
(last modified 2026-08-17T09:53:57+00:00 )
Feb 08, 2017 13:12 UTC
  • Kamanda wa Sepah: Trump ni mwanagenzi, vitisho vya Marekani havina meno

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (Sepah) amesema kuwa wanasiasa wa Marekani wanaelewa vyema kwamba vitisho dhidi ya Iran havina faida yoyote bali vina madhara.

Brigedia Jenerali Muhammad Ali Ja'fari ambaye alikuwa akihutubia Mkutano wa 6 wa Kuenzi Fasihi ya Jihadi na Mapambano katika mji wa Hamedan ulioko magharibi mwa Iran amesema kuwa, katikia kipindi hiki cha maadhimisho ya mwaka wa 38 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu tunaona kuwa kadiri miaka inavyopita ndivyo mapinduzi hayo yanayovyonawiri na kustawi zaidi. Amesema maadui na marafiki wamekiri waziwazi kuhusu nguvu na adhama ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Brigedia Jenerali Muhammad Ali Ja'fari

Brigedia Jenerali Muhammad Ali Ja'fari amesema Rais mpya wa Marekani, Donald Trump ni mwanagenzi na kwamba baadhi ya wachambuzi katika Wizara ya Ulinzi wa nchi hiyo Pentagon wamemnasihi wakimwambia kuwa ulimwengu wa Kiislamu na hata maeneo mengine ya dunia yanaiona Marekani kwenye karatasi tu na kwamba ni dola kubwa linaloelekea kusambaratika.

Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa siri ya kubakia hai Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran tofauti na mapinduzi mengine makubwa duniani ni utambulisho wake wa Kiislamu na kupiga hatua kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu.