Iran yasema Saudi Arabia imechanganyikiwa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i25089-iran_yasema_saudi_arabia_imechanganyikiwa
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, watawala wa Saudi Arabia wamechanganyikiwa na wanawasababishia raia wa nchi hiyo matatizo mengi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 13, 2017 12:02 UTC
  • Iran yasema Saudi Arabia imechanganyikiwa

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, watawala wa Saudi Arabia wamechanganyikiwa na wanawasababishia raia wa nchi hiyo matatizo mengi.

Bahram QasemI, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran katika mahojiano na Televisheni ya Al Alam ameashiria mitazamo ya Saudi Arabia dhidi ya Iran na kusema: "Saudi Arabia inafuata sera za baadhi ya madola makubwa au baadhi ya tawala kama vile utawala wa Kizayuni wa Israel na hivyo kujisababishia hasara kubwa na pia hasara kwa eneo hili na dunia nzima kiujumla."

Qassemi ameongeza kuwa, katika miaka ya hivi karibuni, watawala wa Saudia hawajakuwa na ufahamu sahihi kuhusu Iran na pia kuhusu hali halisi ya eneo hili.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema Saudi Arabia na eneo la Mashariki ya Kati halipasi kufanya kosa la kihistoria baada ya kuja rais mpya wa Marekani. Amesema nchi za eneo hili hazipaswi kuachia madola ya nje ya eneo kuainisha hatima ya Mashariki ya Kati ya Asia Magharibi.

Mrithi wa Kiti cha Ufalme Saudia Mohammad bin Nayef akipokea tuzo kutoka mkuu wa Shirika la Kijesusi la Marekani, CIA.

Kuhusu safari ya hivi karibuni ya mjumbe maalumu wa Kuwait hapa nchini Iran, Qasemi amesema sera za kimsingi za Iran ni kuwa na uhusiano mzuri na nchi jirani na kuongeza kuw auhusiano huo haupaswi kuathiriwa na watu wasiolitakia mema eneo hili yaani madola ya kigeni na utawala wa wa Kizayuni wa Israel.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amegusia pia kuendelea uhasama na uadui wa Marekani dhidi ya Iran katika serikali mpya ya Donald Trump na kusema: "Iran haiogopi uhasama wa Marekani kwani Wamarekani wenywe wanafahamu vyema uwezo wa Iran kwenye eneo la Asia Magharibi." Ameongeza kuwa uwezo wa Iran katika kupambana na maadui hautegemei msaada wa nchi za kigeni.