Mafanikio mapya ya nyuklia ya Iran yazinduliwa na Rais Rouhani
Mafanikio ya karibuni ya nyuklia ya Iran yamezinduliwa na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia.
Awamu ya kwanza ya kituo cha kuzalisha nishati kimezinduliwa katika mkoa wa Qazvin, na huku mradi wa kituo cha kuzalisha dawa za miale ya PET kikizinduliwa katika mkoa wa Alborz na kiwanda cha kwanza cha kuzalisha mawe ya urani kikizinduliwa katika mkoa wa Yazd kwa amri ya Rais Hassan Rouhani wa Iran kupitia mkutano uliofanyika kwa njia ya video. Tarehe 20 mwezi Farvardin wa Kiirani sawa na tarehe 9 mwezi Aprili 2017 Miladia imetajwa kuwa ni Siku ya Taifa ya Teknolojia ya Nyuklia hapa Iran katika kuenzi jitihada kubwa za wasomi wa nyuklia wa Iran na kukamilika mzunguko wa fueli nyuklia.