Viongozi wa kidini: Taifa la Iran litazishinda njama za maadui dhidi yake
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i30282-viongozi_wa_kidini_taifa_la_iran_litazishinda_njama_za_maadui_dhidi_yake
Viongozi wawili wa kidini nchini Iran wenye makao yao mjini Qum wamesisitiza katika taarifa zao walizozitoa kwa nyakati tofauti kwamba, taifa la Iran litazishinda njama za maadui dhidi yake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 10, 2017 03:24 UTC
  • Viongozi wa kidini: Taifa la Iran litazishinda njama za maadui dhidi yake

Viongozi wawili wa kidini nchini Iran wenye makao yao mjini Qum wamesisitiza katika taarifa zao walizozitoa kwa nyakati tofauti kwamba, taifa la Iran litazishinda njama za maadui dhidi yake.

Ayatullah Naser Makarem Shirazi na Ayatullah Hussein Nouri Hamedani wamelaani katika taarifa zao mashambulio ya kigaidi ya Jumatano iliyopita hapa mjini Tehran na kueleza kuwa pamoja na familia za mashahidi na majeruhi wa mashambulio hayo ya kigaidi.

Ayatullah Makarem Shirazi ambaye pia ni  Marjaa Taqlidi amesema kuwa, mashambulio hayo ya kigaidi yamelifanya taifa la Iran kuwa na azma na irada imara zaidi kuliko hapo kabla ya kupambana na makundi ya kigaidi na kitakfiri.

Kwa upande wake Marjaa Taqlidi, Ayatullah Hussein Nouri Hamedani amesema kuwa, Waislamu wanapaswa kudumisha umoja na mshikamano baina yao katika kukabiliana na makundi ya uongo ya kisalafi na kitakfiri ambayo yameletwa na Marekani na utawala haramu wa Israel kwa ajili ya kuzusha hitilafu na mifarakano baina ya Waislamu.

Ayatullah Naser Makarem Shirazi

Amesema kuwa, Wairani watafanikiwa kusambaratisha njama zote za mataifa ya kigaidi ikiwemo Marekani kwa kudumisha umoja na mshikamano baina yao.

Kwa mujizu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, watu 17 waliuawa shahidi na 53 kujeruhiwa katika mashambulio mawili tofauti ya kigaidi ya siku ya Jumatano hapa mjini Tehran yaliyolenga Bunge la Iran na Haram ya Imam Khomeini MA.

Kundi la kigaidi la Daesh limetangaza kuwa, wanachama wake ndio waliohusika na mashambulio hayo mawili ya kigaidi mjini Tehran.