Iran yafuzu fainali kucheza Kombe la Dunia 2018 Russia
(last modified Wed, 14 Jun 2017 04:36:52 GMT )
Jun 14, 2017 04:36 UTC

Timu ya soka ya taifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa timu ya pili kujikatia tiketi ya michuano ya kombe la dunia hapo mwakani huko nchini Russia baada ya kuigaragaza timu ya Uzbekstan mbao 2 kwa nunge.

Mabao kutoka kwa Sardar Azmoun na Mehdi Taremi yalihakikisha Iran, ambayo mkufunzi wake ni Carlos Queiroz, itarejea tena kucheza Kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo ikiwa ni mara ya kwanza kupata mafanikio hayo.

Ushindi wao uliwawezesha kufungua mwanya wa alama nane kati yao na wapinzani wao, ambao wamo nafasi ya tatu kwenye jedwali.

Wachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Iran wakishangilia baada ya mechi

Mabingwa mara tano Brazil walikuwa taifa la kwanza kujiunga na wenyeji Urusi katika kufuzu kwa michuano hiyo ya mwaka ujao nchini Russia.

Timu mbili za kwanza katika kila kundi, kati ya makundi mawili ya kufuzu katika bara Asia zitafuzu, nazo timu zitakazomaliza nafasi ya tatu kila kundi zikutane katika mechi ya muondoano ya kufuzu.