Feb 18, 2018 08:03 UTC
  • Watu wote 66 wafariki dunia katika ajali ya ndege katikati mwa Iran

Watu 66 wamefariki dunia katikati mwa Iran baada ya ndege ya abiria kuanguka asubuhi ya leo.

Ndege hiyo ya Shirika la Aseman ilitoweka katika rada leo saa mbli asubuhi ikiwa inasafiri kutoka Uwanja wa Ndege wa Mehrabad mjini Tehran kuelekea mji wa Yasuj ambao ni mji mkuu wa mkoa  wa Kohgiluyeh na Boyer-Ahmad kusini magharibi mwa Iran.

Ndege hiyo aina ya ATR 72 ilitoweka kwenye rada  dakika 20 hivi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Tehran. Ndege hiyo imeanguka katika eneo la Semirom katika mkoa wa Isfahan kati mwa Iran na shughuli za uokoaji zinaendelea. Maelezo zaidi yatakujieni baadaye.

 

Tags