Rais wa Iraq: Uhusiano wa Tehran na Baghdad ni mzuri
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i47554-rais_wa_iraq_uhusiano_wa_tehran_na_baghdad_ni_mzuri
Rais wa Iraq amevitaja vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni kwa madhara ya serikali na wananchi wa Iraq.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Aug 20, 2018 03:55 UTC
  • Rais wa Iraq: Uhusiano wa Tehran na Baghdad ni mzuri

Rais wa Iraq amevitaja vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni kwa madhara ya serikali na wananchi wa Iraq.

Akizungumza katika mahojiano maalumu wiki hii na televisheni ya al Aalam yenye makao yake hapa Tehran, Rais Fuad Maasum wa Iraq ameashiria hatua ya upande mmoja ya Marekani dhidi ya Iran na kuanza tena vikwazo dhidi ya Tehran na kuongeza kuwa: Vikwazo hivyo si tu vitaiathiri Iraq bali pia vitakuwa kwa madhara ya nchi zote zilizosaini makubaliano ya nyuklia ya JCPOA  na Marekani.  

Bendera za Iran na Iraq

 

Rais wa Iraq ameashiria uhusiano kati ya Tehran na Baghdad na kubainisha kuwa haiwezekani Marekani kuitumia Iraq kama wenzo dhidi ya upande mwingine. Fuad Maasum amesisitiza pia juu ya kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili za Iran na Iraq na kueleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangu siku ya kwanza ya kuendesha maopambano dhidi ya magaidi wa Daesh huko Iraq si tu imetoa misaada ya kbinadamu pekee bali hata misaada ya kijeshi na kiitelijinsia. Makundi na mirengo mbalimbali ya kisiasa nchii Iraq katika wiki kadhaa zilizopita yaliyoa taarifa kwa nyakati tofauti yakilalamikia hatua za Marekani dhidi ya Iran na kusisitiza kuwa taifa la Iraq linawaunga mkono wananchi wa Iran.

Rais Donald Trump wa Marekani tarehe Nane mwezi Mei mwaka huu alitangaza kujitoa nchi hiyo katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kurejeshwa vikwazo dhidi ya Iran; hatua ambayo imetajwa kuwa ni ya upande mmoja na iliyo kinyume cha sheria. Tarehe Sita mwezi huu wa Agosti pia Rais wa Marekani aliamuru kurejeshwa baadhi ya vikwazo vya nchi hiyo dhidi ya Iran vilivyo kinyume cha sheria vinavyohusiana na sekta ya uuandaji magari na dhahabu.