Qassemi: Magaidi watashindwa kulipiza kipigo walichopata Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i49451-qassemi_magaidi_watashindwa_kulipiza_kipigo_walichopata_iraq
Iran imelaani na kulitaja kuwa la kinyama shambulio la kigaidi lililofanywa katika mji wa Mosul kaskazini mwa Iraq na kueleza kuwa magaidi watagonga mwamba katika juhudi zao za kujaribu kulipiza kisasi kipigo walichopata kutoka kwa serikali na wananchi wa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 12, 2018 04:30 UTC
  • Qassemi: Magaidi watashindwa kulipiza kipigo walichopata Iraq

Iran imelaani na kulitaja kuwa la kinyama shambulio la kigaidi lililofanywa katika mji wa Mosul kaskazini mwa Iraq na kueleza kuwa magaidi watagonga mwamba katika juhudi zao za kujaribu kulipiza kisasi kipigo walichopata kutoka kwa serikali na wananchi wa nchi hiyo.

Bahram Qassemi Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema kuwa masalia ya makundi ya kigaidi yamekusudia kulipiza kisasi dhidi ya serikali na wananchi wa Iraq kwa kutekeleza vitendo vya kikatili na kigaidi dhidi ya raia wasio na hatia wa nchi hiyo. Qassemi amesema magaidi kamwe hawatashinda na kwamba wataangamizwa kikamilifu katika eneo hilo karibuni hivi.

Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran

Watu wasiopungua watano walipoteza maisha na wengine 14 kujeruhiwa Alhamisi iliyopita baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu kulipuka karibu na mji wa Mosul katika shambulio la kigaidi la nadra kushuhudiwa tangu kuangamizwa mjini humo magaidi wa kundi la kitakfiri la Daesh mwaka uliopita. Mlipuko wa bomu la kutegwa garini ulitokea usiku katika mkahawa mmoja huko Mosul; mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq.  

Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulio hilo la Mosul hata hivyo magaidi wa Daesh wamekuwa wakifanya mashambulizi kama hayo ya kuvizia huko Iraq baada ya kupoteza udhibiti wa maeneo mengi ya nchi hiyo.