Rouhani: Kwa azma, taifa la Iran litaweza kuvuka vikwazo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i51813-rouhani_kwa_azma_taifa_la_iran_litaweza_kuvuka_vikwazo
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema watu wa Iran kwa irada, wanaweza kuvishinda vikwazo na kuvuka matatizo yote yaliyopo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 26, 2019 11:13 UTC
  • Rouhani: Kwa azma, taifa la Iran litaweza kuvuka vikwazo

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema watu wa Iran kwa irada, wanaweza kuvishinda vikwazo na kuvuka matatizo yote yaliyopo.

Rais Rouhani ameyasmea hayo leo Jumanne mjini Tehran katika kikao cha kila mwaka cha Benki Kuu ya Iran ambapo amesema kuwa, Marekani imetumia uwezo wake wote kuuwekea vikwazo mfumo wa benki wa Iran na pia imeiwekea Iran vikwazo vya mafuta na sekta nyingine nyingi za uchumi. Ameongeza kuwa, wizara za mambo ya nje, mafuta na Benki Kuu ya Iran ziko mstari wa mbele katika kukabiliana na mashiniklizo ya kiuchumi ya Marekani.

 

Rais Rouhani amesema ni jambo linalotarajiwa kuwa katika hali hii ya vikwazo, mlingano wa kibiashara nchini utakuwa si mzuri lakini pamoja na hayo katika kipindi cha miezi 11 iliyopita, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeweza kuuza nje bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 40 na kununua kutoka nje bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 38.

 

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ameendelea kusema kuwa, Iran imefanikiwa kufanya kazi kubwa katika eneo na kuongeza kuwa: "Sehemu ya kazii hii imefanywa na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu pamoja na  Wizara ya Mambo ya Nje na sehemu nyingine imefanywa na sekta ya kiuchumu ya Iran na jambo hili linaonyesha kuwepo mshikamano baina ya sekta mbali mbali nchini.

 

Rais Rouhani ameashiria pia safari ya Rais Bashar al Assad wa Syria siku ya Jumatatu mjini Tehran na kusema: "Rais wa Syria ametembelea Iran kwa lengo la kutoa shukrani kwa taifa la Iran, serikali na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.