Rouhani: Iran inataka kupanua uhusiano na nchi zote jirani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i52230-rouhani_iran_inataka_kupanua_uhusiano_na_nchi_zote_jirani
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran ina hamu ya kuwa na uhusiano mzuri na majirani zake na kuongeza kuwa, matatatizo yaliyopo na baadhi ya nchi yameanzisha nchi hizo zenyewe.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 17, 2019 21:47 UTC
  • Rouhani: Iran inataka kupanua uhusiano na nchi zote jirani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa Tehran ina hamu ya kuwa na uhusiano mzuri na majirani zake na kuongeza kuwa, matatatizo yaliyopo na baadhi ya nchi yameanzisha nchi hizo zenyewe.

Dakta Hassan Rouhani ameyasema hayo katika hadhara ya wananchi wa Bushehr huko kusini mwa Iran na kusema lengo la Iran ni kuwepo maendeleo na ustawi katika eneo zima na Magharibi mwa Asia. Ameongeza kuwa, Iran ina uhusiano mwema na majirani zake kama Qatar, Oman, Uturuki, Jamhuri ya Azerbaijan, Turkmenistan, Afghanistan na Pakistan na inataka kuwa na uhusiano mzuri na nchi zote jirani.

Rouhani ameashiria safari yake nchini Iraq na kusema: Uhusiano wa Iran na Iraq ni wa kupigiwa mfano katika kanda hii na duniani kote. Rais wa Iran amesema kuwa, safari yake ya siku tatu nchini Iraq na makubaliano yaliyofikiwa na nchi hiyo yana maana kuwa, uhusiano wa Tehran na Baghdad si uhusiano baina ya serikali za nchi mbili pekee, bali ni uhusiano wa matabaka, makundi na viongozi wa kisiasa, kijamii na kidini wa pande hizo mbili.

Rais Hassan Rouhani

Vilevile amezungumzia njama zinazofanywa na maadui kwa ajili ya kutoa pigo kwa Iran na kusema: Licha ya njama zinazofanywa na Marekani, Wazayuni na baadhi ya nchi vibaraka wa kanda hii kwa ajili ya kuwashinikiza wananchi wa Iran lakini kamwe hawataweza kulipigisha magoti taifa kubwa la Iran.