Rouhani: Taifa la Iran litamshinda adui yeyote yule
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53264-rouhani_taifa_la_iran_litamshinda_adui_yeyote_yule
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia njama za maadui dhidi ya Tehran na kusisitiza kuwa, taifa hili la Kiislamu litamshinda adui yeyote yule kwa mshikamano wake, kusimama kidete na kuwa na matumaini na mustakbali mwema.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
May 04, 2019 03:45 UTC
  • Rouhani: Taifa la Iran litamshinda adui yeyote yule

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia njama za maadui dhidi ya Tehran na kusisitiza kuwa, taifa hili la Kiislamu litamshinda adui yeyote yule kwa mshikamano wake, kusimama kidete na kuwa na matumaini na mustakbali mwema.

Rais Hassan Rouhani amesema hayo leo hapa mjini Tehran katika sherehe za kuenzi na kutukuza nafasi ya mwalimu na huku akiashiria malengo ya Marekani ya kutoa vitisho na kuiwekea vikwazo Iran amesema, Iran yenye hadhi, huru na yenye taathira katika eneo hili na dunia nzima siyo inayotakiwa na Marekani.

Amesisitiza kuwa, msingi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kulifanya taifa la Iran liwe huru katika hali zote, lakini maadui hasa Marekani hawafurahishwi na jambo hilo. Amesema, Marekani inafanya njama za kupunguza kiwango cha fedha za kigeni za Iran ili ifikie malengo yake haramu, hata hivyo lakini Jamhuri ya Kiislamu imejipanga vizuri kukabiliana na njama hizo.

Mapatano ya nyuklia ya JCPOA baada ya kujitoa Marekani

 

Rais Rouhani amegusia pia hatua ya Marekani ya kuondoa msamaha kwa baadhi ya nchi kununua mafuta ya Iran na kusema, taifa la Iran linaendelea kuuza mafuta yake kama kawaida na halizuiwi na vikwazo hivyo vya Marekani.

Amegusia pia njama za tawala za Kizayuni na Aal Saud za kujaribu kukwamisha utekelezaji wa mapatano ya nyuklia ya JCPOA na kusema kuwa, serikali ya hivi sasa ya Marekani inachukua hatua zake kwa kurubuniwa kwa fedha za makundi yenye misimamo mikali ya kibaguzi ya Wazayuni na Aal Saud.