Kharrazi: Madola ya Ulaya yanapaswa kuonyesha 'irada' ya kulindwa makubaliano ya JCPOA
(last modified Mon, 13 May 2019 03:38:13 GMT )
May 13, 2019 03:38 UTC
  • Kharrazi: Madola ya Ulaya yanapaswa kuonyesha 'irada' ya kulindwa makubaliano ya JCPOA

Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, madola ya Ulaya yanaweza kuonyesha nia na irada yao ya kutaka kuhifadhiwa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kwa kutekeleza ahadi zake kama kutekelezwa haraka mfumo maalumu wa kifedha wa Ulaya na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (INSTEX).

Sayyid Kamal Kharrazi, Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  amesema hayo mjini Paris Ufaransa katika mkutano uliohudhuriwa na baadhi ya viongozi wa vituo muhimu vya kifikra nchini humo ambapo amekosoa vikali kigugumizi cha madola ya Ulaya katika kutetekeleza ahadi zake kuhusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. 

Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran  amebainisha sababu za uamuzi wa hivi karibuni wa Iran wa kusitisha baadhi ya ahadi zake kwa mujibu wa makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA na kueleza kuwa, uamuzi huo wa Tehran ni haki yake ambayo inatambuliwa na makubaliano hayo.

Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Kigeni wa Umoja wa Ulaya

Aidha Kamal Kharrazi amelitaja pendekezo la Rais Donald Trump wa Marekani la kufanya mazungumzo na Iran kwamba, ni propaganda tupu ambazo zinapaswa kupuuzwa.

Aidha Mkuu wa Baraza la Kistratijia la Uhusiano wa Nje la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, hatua ya Trump ya kuitoa nchi yake katika makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na kisha kuwatwisha wananchi wa Iran vikwazo mbalimbali na vya kidhumla haijaacha nafasi ya kuweko mazungumzo au kuiamini Marekani.

Tags