Baqeri: Maandamano ya Quds yatasambaratisha njozi za Marekani kuhusu Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53820-baqeri_maandamano_ya_quds_yatasambaratisha_njozi_za_marekani_kuhusu_palestina
Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema maandamano makubwa yatakayoshuhudiwa leo Ijumaa katika Siku ya Kimataifa ya Quds yatasambaratisha njozi na ndoto za alinacha za Marekani dhidi ya taifa la Palestina.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 31, 2019 05:58 UTC
  • Baqeri: Maandamano ya Quds yatasambaratisha njozi za Marekani kuhusu Palestina

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema maandamano makubwa yatakayoshuhudiwa leo Ijumaa katika Siku ya Kimataifa ya Quds yatasambaratisha njozi na ndoto za alinacha za Marekani dhidi ya taifa la Palestina.

Meja Jenerali Muhammad Hossein Baqeri alisema hayo jana Alkhamisi na kufafanua kuwa, "Bila shaka maandamano makubwa ya mwaka huu ya Siku ya Quds yatakuwa nembo ya aina yake ya kuhuisha kiapo cha kufungamana na kadhia tukufu ya Palestina, kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina sambamba na kuulaani utawala ghasibu, bandia na wa Kizayuni wa Israel."

Amebainisha kuwa, bila shaka maandamano ya leo yatakuwa chachu ya kutupa katika kaburi ya sahau mpango wa Marekani uliopewa jina la "Muamala wa Karne" wenye lengo la kuitokomeza kadhia ya Palestina.

Maandamano ya Siku ya Kimataifa ya Quds kufanyika leo kote duniani

Mkuu wa Vikosi vya Ulinzi vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, Marekani inataka kuutumia mpango huo kufanikisha ndoto zake za kuwepo "Mashariki ya Kati Kubwa" na "Israel kuanzia Mto Nile Hadi Furati" njama ambazo bila shaka zitagonga mwamba.

Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, hayati Imam Ruhullah Khomeini kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds na kwa msingi huo wakuu wa mihimili mitatu ya dola, maafisa wa taasisi mbalimbali za nchi na viongozi wa jeshi, shakhsia mbalimbali wa kidini na kisiasa wametoa taarifa mbalimbali wakiwataka wananch kushiriki kwa wingi katika maandamano ya leo.